Saturday, November 17, 2007

UTEUZI WA ZITO KABWE, NI FUMBO, KITENDAWILI AU HADITHI?

Fumbo, kitendawili na hadithi kwa pamoja?

Kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi wake wa kuunda tume ya kuchunguza suala zima la mikataba ya madini nchini, na napenda ifahamike kuwa pongezi hizi ni za dhati kwa maana ya kutoka moyoni, tena kule kilindini. Pongezi hizi ni kwa sababu mbili.

Kwanza ni kwa sababu ya rais kutimiza ahadi aliyoahidi hivi karibuni katika mkutano mkuu wa CCM pale Dodoma, aliahidi kufanya hivyo, naam amefanya tena kwa muda mfupi sana, ametimiza ahadi.

Lakini la pili lililokubwa zaidi ni kwa vile rais anaelekea kupona ule ugunjwa wa siku nyingi wa serikali ya CCM kufanya mambo kwa kuzingatia maslahi ya chama zaidi kuliko Taifa, uginjwa wa kudhani wapinzani hawawezi kutoa mchango wowote kwa serikali iliyoko madarakani zaidi ya kupiga kelele za majukwaani na kupoteza muda, hiyo ndio ilikuwa pengine ni dhana ya CCM na serikali kwa ujumla.

Lakini Kikwete ananishawishi nianze kuamini kuwa CCM (kama si dhamira binafsi ya Kikwete) inaelekea kupona uginjwa huu, ni pale alipoamua kuunda tume inayojumuisha viongozi wa CCM na wale wa upinzani wakiwamo John Momose Cheyo wa UDP na Zito Zuberi Kabwe wa CHADEMA. Kwa moyo mkunjufu nasema hongera sana Mheshimiwa rais na asante!

Hata hivyo mwishoni mwa makala hii nitakutaka mpendwa msomaji wangu uamue/upembue uteuzi huu, ikiwa ni fumbo, kitendawili au hadithi kwa maana ya historia mpya ambayo vizazi vitasimuliwa hapo baadae?

Tume hii imekuwa gumzo mitaani na hasa kwa wafuatiliaji wa masuala mbalimbali hapa nchini, na aliyesababisha gumzo hilo si mwingine ni Zitto Kabwe, suala sio tume, suala ni Kabwe kuwa kwenye tume hiyo. Wakati gumzo hilo likiwa bado bichi, gazeti moja likaripoti kuwa baadhi ya wanachama wa CHADEMA wamanza kumjadili Kabwe, kwamba inakuwaje awe kwenye tume hiyo na mambo mengine mengi ambayo nimeyatafsiri kama ya kitoto kama sio propaganda za baadhi ya maadui wa Zitto Kabwe kupitia magazeti hayo. Suala la Zitto kabwe kuwa kwenye tume hiyo siyo suala la kiitikadi, ni swala la kitaifa.

Mimi sijui kwa upande wako unafikiriaje, wenzako wanasema Zitto Kabwe ana ajenda ya siri na CCM, kwamba ananunuliwa ili kuzibwa midomo, mimi nayakataa madai haya kwa nguvu zote, ni utoto wa kimawazo kuanza kufikiri hivi mapema, tusiache kujadili hoja ya msingi, tukianza kujadili uhalali wa Kabwe kuchaguliwa na rais anayetokea CCM tutawapa walfi nafasi ya kupumua kama wapo.

Na hapa leo nataka nikutafakarishe wewe mwenye mawazo hayo ya kitoto kuhusiana na uwepo wa Kabwe kwenye tume ya rais.

Unakumbuka kuwa Zitto Kabwe alifungiwa na Bunge (spika?) kuhudhuria vikao vya bunge kwa madai ya kulidanganya bunge, kwamba alitoa madai ya uongo, wengine wakafika mbali kwamba amemdhalilisha Waziri Karamagi? Unafikiri hii ina maana gain? Sikiliza wewe! tungeweza kumwita Kabwe ni mhalifu aliyeko kifungoni, lakini mpaka anatoka bungeni alisisitiza kuwa madai yake yalikuwa kweli, na akasema anawaachia wananchi wengine waamue, kwamba yeye alikuwa amemaliza zamu yake. Bunge likazodolewa na kushutumiwa na wanasiasa, wanaharakati na wananchi wengine wa kawaida. Ninakumbuka wakati ule nilikuwa Mbeya, nilipigiwa simu na mwanafunzi mmoja wa sekondari iliyoko Morogoro, huyu msichana alisema hivi, “niliiheshimu sana CCM, lakini sasa kwa hatua ya Bunge kumfungia Zito Kabwe, mh, mimi nahamia CHADEMA” Nilichomshauri ni kutulia ili afanye maamuzi sahihi, kuhama chama kusingemnusuru Zitto Kabwe wakati ule.

Zitto Kabwe aliitwa muongo, mzushi, wakasema anajitafutia umaarufu kwa kusema uongo, mjidala hiyo ikafika hata vyuoni na kuwagawa wanafunzi, wengine wakimtetea huku wengine wakimshutumu na kumwita kimbelembele, Zitto akasonga mbele, vyama vya upinzani vikachochea moto kwa kuamua kupanga ziara za kwenda kuishitaki serikali kwa umma, maana bunge lilishindwa kuidhiti serikali.

Mbele ya macho ya bunge Kabwe alikuwa ni mhalifu aliyeko kifungoni, kadhalika mbele ya Karamagi na Kikwete na baadhi ya wana CCM, sina shaka kwamba adhabu ya bunge kwa Zitto ilimfariji sana Karamagi aliyemwita Zitto Kabwe kuwa ni muongo na mdhalilishaji.

Wiki iliyopita limetokea jambo, sijui mpaka saa niliiteje, ninakupa nafasi ya kutoa jina. ‘Mhalifu’ yule yule, muongo, mzushi na mdhalilishaji aliyefungiwa kwa misimamo yake kwenye kulinda rasilimali za Taifa na hasa madini, leo amekuwa wa maana mbele ya rais hata kupewa ujumbe katika tume yenye kazi ya kuchunguza suala lile lile la madini. Unasemaje? Je, rais kapitiwa au anajua kwa hakika alichokifanya? Hajui kuwa Zito ni mfungwa? tena kwa sababu ya kutetea madini ya nchi yetu, madini ambayo yamefanya serikali ipoeze imani kwa wananchi wake? Rais amesahau kuwa waziri wake (Karamagi) anamchukulia kuwa Zito Kabwe ni muongo na mzushi? Kwa nini kaamua kumteua? Je, Zitto Kabwe ni msafi tofauti na anavyoonekana mbele za macho ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Je Zito Kabwe ni mkweli tofauti na fikra za Karamagi? Au kwa nini rais amemteua? Kwetu tunaamini kuwa mheshimiwa rais kazingatia na kuamini kuwa Zito Kabwe anafaa na anaiweza kazi aliyompa, kigezo cha uadilifu, uchapa kazi, ukweli na uwazi ndicho kilichompa kibali zito mbele za rais Kikwete.

Kama ndivyo basi, tuiteje uteuzi huo, ni fumbo la rais kwa Karamagi na bunge? Kwa maana kwamba bunge na Karamagi walivyomfikiria Zitto Kabwe sivyo alivyo? Au ni vipi? Kama ndivyo, je rais amemsuta Karamagi? Kwa hiyo kama ni hivyo, huo si ushindi wa kishindo kwa Zitto Kabwe kama mwanaharakati, kwamba sasa imethibitika kuwa alikuwa ni Nabii asiyeheshimika na kutiliwa mashaka bure tu!

Je hatuwezi kufikiri kuwa CCM na serikali yake imejizodoa? Mimi huko simo, ni katika kujaribu kuwaza na kuwazua, lakini pongezi zangu kwa rais zinabaki palepale!
Ni vipi pia? Uteuzi huo ni kitendawili? Nani atakitegua? Kinasemaje hicho kitendawili? Je ni hadithi mpya katika historia ya Tanzania?

Suala la Zito kwenye tume hiyo limenikumbusha habari za RADA, wanaharakati walipotuhumu kuwa ina mazingira ya rushwa, baadhi ya wanunuzi wakapinga kwamba sivyo ilivyokuwa. Leo TAKUKURU imemtangaza mmoja wa watuhumiwa hao wa rushwa hadharani, hii ina maana kuwa mazingira ya rushwa yalikuwapo, je wanasemaje wanaposikia kuwa madai ya wale walioitwa wazushi yamethibitika kuwa na ukweli?

Naamini hili ni funzo hata kama rais amefanya bila kujua kuwa kuna watu wangekuja na tafsiri nyingi sana baada ya uteuzi huo.Kwa hiyo tunashawishika kuamini kwamba, kumbe kuna madai mengi ya wapinzani yakiwemo yale ya ufisadi tutakuja kuujua ukweli wake siku moja, tena watakaokuja kuuthibitisha ni hao hao wahusika, tuombe Mungu!

Kila la Heri tume ya rais!

Saturday, July 21, 2007

Happy Birthday Madiba

Mzee Nelson Rolihlahla Madiba Mandela

Naandika makala hii kwa heshima kubwa ya mwanaharakati chipukizi kabisa, mwanafunzi wa sekondari, Elizabeth David wa Arusha. Ni moja ya hazina zinazochipuka kwa taifa hili wakiwa na moyo wa uzalendo kwa Taifa hili, nikipata nafasi nitaeleza kirefu kuhusu yeye.

Leo namzungumzia Nelson Rolihlahla Madiba Mandela, kwangu huyu ni mmoja kati ya zawadi ambazo Mungu aliamua kuutunuku ulimwengu, namwita shujaa na hilo halihitaji ufafanuzi wala wakati wa mjadala. Maisha yake yanajieleza.

Alizaliwa kitongoji cha Transkei nchini Afrika ya Kusini tarehe 18, julai 1918, hii ina maana kwamba wiki iliyopita tarehe 18, jumatano mwana huyu wa Afrika alitimiza miaka 89. Kwa faida ya wasomaji wa safu hii, shujaa huyu alizaliwa na baba ambaye alikuwa chifu wa kabila la Watembu, aliitwa Henry mandela.

Miongoni mwa mambo mengi ambayo pengine wengi wetu hatuji labda kwa sababu hayajaripotiwa sana, ni kwamba kwa taaluma Mandela ni mwanasheria aliyehitimu shahada yake katika chuo kikuu cha Witwatersrand mwaka 1942 kabla hajawa mwanasiasa kwa kujiunga na ANC mwaka 1944

Kuishi maisha ya miaka 89 katika ulimwengu huu uliochanganyikwa si kitu kidogo hasa kwa mtu kama mandela aliyepitia karibu robo ya maisha yake. Kati ya misukosuko ikiwemo kuwekwa gerezani kwa miaka ipatayo 27.

Unaweza kumwita Mandela shujaa, jasiri, mapambanaji au mwanamapinduzi. Alipinga uonevu wa kila namna, alikataa ukandamizaji na aina ya maisha ya watu waliotaka kujifanya miungu wa dunia hii. Kwa nini nasema haya yote! Sikiliza mandela alivyosema mwenyewe:

Anasema “Nimepinga utawala wa watu weupe, nimepinga utawa wa watu weusi. Nimeheshimu mpango wa kidemokrasia na jamii iliyo huru ambapo watu wote wataishi pamoja kwa amani pamoja na fursa sawa. Ni mpango ambao nitaishi kwa ajili hiyo na kuufanikisha. Lakini ikibidi, basi ni mpango ambao nimejiandaa kufa kwa ajili yake”

Maneno haya ni mazito sana, Mandela aliyasema haya alipohukumiwa kifungo cha miaka mitano katika kesi fulani hivi, eti kwa kosa la uhaini, lakini uhaini uliodiwa na maadui zake ni kile kitendo cha yeye kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini. Hiyo ni mwaka

Kwa wale amabo wamefuatilia maisha ya harakati ya Madiba wanaweza kukubaliana na mawazo yangu kwamba Mandela hakuwa tu msemaji bali pia mtu wa vitendo, na si hivyo tu bali pia alianza kutenda kabla ya kusema, upo hapoo? Baada ya kutafakari hayo, nikajikuta nakumbuka aya fulani ya Biblia inayosema “kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha” Matendo 1:1 Unaona hapo, watu wanaanza kutenda na kisha kusema au kufundisha.

Je wakoje wanasiasa wetu wa leo, unaweza kuwafananisha na Mandela? Je wanamfikia hata kwa mbali? Wangapi angalau wanatenda wanachokisema? Mandela alianza kutenda kabla hajasema, alianza kupigania uhuru wa waafrika hata kabla Afrika haijajua dhamiri yake, kabla waafrika hawajajua, kabla hatamka hadharani kuwa amejitolea maisha yake kuipigania Afrika!

Kwa nini nasema kuwa alianza kutenda kabla hajasema? Tuirejee kwanza sehemu ya kauli yake “Ni mpango ambao nitaishi kwa ajili hiyo na kuufanikisha. Lakini ikibidi, basi ni mpango ambao nimejiandaa kufa kwa ajili yake”

Angalia maisha yake kabla ya kuwekwa gerezani, alipigania uhuru wa weusi, kitu ambacho wazungu walikitafsiri kama uhaini na hivyo kumtupa lupango.

Je, alipigana kabla ya kutoa kauli hiyo gerezani?
Ndiyo, hii ni bada ya chama chake cha ANC kupigwa marufuku kuendelea kuwapo nchini Afrika ya Kusini mwaka 1960. Je Mandela akaishia hapa? Hapana, kitendo cha ANC kufungiwa kilichochea moto wa harakati za mandela kwani kwa ushawishi wake baadhi ya maodfisa wa ANC walikubali kuunda kikundi kingine cha harakati za ukombozi kilichojulikana kwa jina la Umkhonto we Sizwe kikiwa na malengo yale yale ya ANC, wao walikitafsiri kikundi hiki kama ubawa (wing) wa ANC. Kwa kitendo hicho, ilipofika mwaka 1962, Mandela alikamatwa na kuhukumiwa kifungo miaka mitano pamoja na kazi ngumu akiwa gerezani, hatia kubwa kwa mujibu wa wazungu ni kwamba, eti Mandela alikuwa akitaka kuipundua serikali yao nchini humo. Ndio maana nasema alianza kupambana kwa ajili ya ndugu zake waafrika, hata kabla hajawaambia kuwa atapambana kwa ajili yao! Tuko pamoja?

Mwaka 1964, July, 14, Mandela na wenzake walihukumiwa kifungo cha maisha. Kitendo hicho kilikuwa kama kinauamsha ulimwengu kuanza kujua hasa Mandela alikuwa nani kwa Waafrika.

Nelson Mandela aliachiwa huru februal 11, 1990 . Je aliacha kutekeleza ahadi yake kwa waafrika? Hapana kwani kwa moyo wake wote akajikita zaidi katika mapamano kama alivyokuwa ameahidi, alipigfania kutimiza ndoto zake. Ndoto gani? Alisema hivi “Nimepinga utawala wa watu weupe, nimepinga utawa wa watu weusi. Nimeheshimu mpango wa kidemokrasia na jamii iliyo huru ambapo watu wote wataishi pamoja kwa amani pamoja na fursa sawa. Ni mpango ambao nitaishi kwa ajili hiyo na kuufanikisha. Lakini ikibidi, basi ni mpango ambao nimejiandaa kufa kwa ajili yake”
Ndio maana mwaka 1991, katika kongamano la kwanza la ANC, Mandela alichaguliwa kuwa rais wa ANC huku swahiba wake Oliver Tambo akiwa Mwenyekiti.

Tangu wakati huo, Mandela hajaacha kupambana, wiki iliyopita huku akiadhimisha miaka 89 ya kuzaliwa kwake, alizindua kikundi cha viongozi mashuhuri, wazee wenye hekima duniani kikiwa na lengo la kutatua matatizo yanayoikabili dunia kwa sasa.n Kikundi hiki kikiongozwa na Mandela mwenyewe kwa kusaidiana na mkewe Graca Machel na mwenyekiti wake, Askofu mkuu mstaafu, Desmond Tutu watatumia hekima walizojaaliwa na mwenyezi Mungu kuikwamua dunia kutoka mahali pabaya ilipofika. Unaweza kuona sasa, kwamba Mandela bado anapambana.

Swali langu ni hili, je viongozi wetu wa leo watakuaje watakapofika umri huu wa Mandela? Je watakumbukwa na kuenziwa kama tunavyomuenzi mzee huyu? Mbona baadhi yao wameanza kuchokwa na watu wao, majimboni, wilayani, na kwinginekeo wakati hata miaka 60 bado? Hii ni changamoto, Mandela hajatumia uchawi, uchawi wake mkubwa ni moyo wake wa kujitoa kwa ajili ya watu wake, na wala sio kujaza matumbo tu kwa kula vya wananchi.

Nilikwambia naandika makala hii kwa heshima kubwa kabisa ya wanaharakati akiwemo binti mdogo Elizabeth David, je wao watakuwaje? Kwa mfano, Elizabeth anampend sana Mandela, basi ni vizuri akatamani pia moyo wa Mandela, ili afanikiwe na kisha kuenziwa baadae!

Nimalizie kwa kumtakia kila la heri, mzee Nelson Rolihlahla Madiba Mandela, heri yake ya siku ya kuzaliwa!